Junior School Learning
Simple, clear, and engaging learning materials for junior school learners.
Utangulizi wa Fasihi ya Junior School
Fasihi ni sanaa inayotumia lugha kwa ubunifu ili kuwasilisha mawazo,hisia na ujumbe unaomhusu mwanadamu pamoja na jamii anamoishi.Fasihi hutusaidia kuelewa maisha, tabia na tamaduni za watu.
Kwa sababu hii,fasihi hufahamika kama kioo cha jamii kwa kuwa huonyesha maisha halisi ya binadamu.
Umuhimu wa Fasihi kwa Wanafunzi
Fasihi ina mchango mkubwa katika maendeleo ya mwanafunzi;
Kupitia fasihi, mwanafunzi huimarisha matumizi ya lugha na kukuza fikra pana.
Fasihi pia humfundisha mwanafunzi maadili mema, kumsaidia kuelewa jamii yake,kukuza ubunifu na kujenga uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha na kujiamini.
Aina za Fasihi
Fasihi ina tanzu mbili kuu;
1.Fasihi Simulizi
2.Fasihi Andishi
Fasihi Simulizi
Fasihi simulizi ni fasihi inayorithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mdomo.Haijaandikwa bali husimuliwa, kuimbwa au kuchezwa.
Baadhi ya vipengele vya fasihi simulizi ni kama, Hadithi,Nyimbo, Semi, Maigizo na Mazungumzo.
Fasihi Andishi
Fasihi andishi ni fasihi iliyoandikwa na kusomwa kwa maandishi. Fasihi hii huhifadhiwa katika vitabu au maandiko mengine.
Baadhi ya vipengele vya fasihi ni kama, Ushairi Andishi, Tamthilia na Novela.
Sehemu Muhimu katika Fasihi Simulizi ya Junior school
Fasihi simulizi katika shule za Junior School huhusisha Hadithi, Nyimbo, Mazungumzo, na semi.
Hadithi
Hadithi ni masimulizi ya kubuni au ya kweli yanayosimuliwa ili kuburudisha,kufundisha au kuonya jamii.Hadithi hutumia wahusika kama binadamu,wanyama au viumbe wa kufikiria.
Hadithi husaidia wanafunzi:
- Kujifunza maadili
- Kuimarisha lugha
- kukuza ubunifu na fikra
Aina za Hadithi
Kuna aina mbalimbali za hadithi katika fasihi simulizi ambazo tunasoma katika Junior School.Baadhi ya aina hizo ni:
- Mighani
- Hekaya
- Hurafa
- Visasili
Kila aina ya hadithi ina sifa na umuhimu wake katika jamii.
Hurafa
Hurafa ni aina ya hadithi ambayo mara nyingi hutumia wanyama au viumbe wa kubuni kama wahusika wakuu.Husimuliwa hususani watoto.
Hurafa huwa na:
- Maudhui ya kufurahisha
- Mafunzo ya maadili
- Mwisho unaotoa mafunzo
Sungura na Kobe
Hapo zamani za kale, kulikuwa na Sungura ambaye alikuwa akijisifu sana kwa kasi yake.Kila siku alimdhihaki Kobe, akimwambia kuwa alikuwa mlegevu na hafai kushindana na yeyote.
Siku moja , Kobe alimchokoza Sungura kwa kumwambia,
“Usivune sana,hata polepole inaweza kushinda.”
Wakaamua kufanya mashindano ya mbio.Sungura alianza mbio kwa kasi kubwa sana na akamuacha kobe mbali.Akiwa njiani, sungura aliona ameshinda tayari, akaamua kupumzika chini ya mti na kulala.
Kobe aliendelea kutembea taratibu bila kusimama.Alipofika mwisho wa mbio,Sungura bado alikuwa amelala.Kobe akashinda mashindano hayo.Sungura aliamka akiwa ameshindwa na akajifunza somo muhimu..
Hadithi yangu imeishia hapo.
Sifa za Hurafa
- Wahusika wake mara nyingi ni wanyama
- Hutumia lugha rahisi
- Huwa na fomula maalum ya kuanzia
- huwa na fomula maalum ya kumalizia
- Huwa na funzo mwishoni
Umuhimu wa Hurafa
- Huburudisha wasikilizaji
- Hufundisha maadili mema
- Hukuza fikra na ubunifu wa wanafunzi
- huifadhi tamaduni za jamii
Mighani
Mighani ni hadithi za kishujaa.Hadithi hizi humhusu shujaa anayejitokeza kulinda jamii,kupigana na maadui au kufanya vitendo vya ujasirri wahali ya juu ila anasalitiwa na mtu wake wa karibu.
Mighani hutumiwa:
- Kukuza uzalendo na ujasiri
- Kufundisha maadili ya jamii
- Kuhifadhi historia na utamamaduni
Shujaa Liyongo
Zamani za kale, aliishi shujaa mmoja aliyejulikana kam aLuanda Magere. Alikuwa suhujaa mwenye nguvu nyingi na mwili uliokuwa mgumu kama jiwe. Hakuna silaha iliyoweza kumdhuru.
Luanda Magere aliilinda jamii yake dhidi ya maadui. Kila adui aliyemshambulia alishindwa kwa urahisi. Kwa sababu ya nguvu zake, Watu walimheshimu na kumuogopa kwa wakati mmoja.
Hata hivyo, siri ya nguvu za Luanda Magere haikuwa mwilini mwake wote. Alikuwa na sehemu moja tu dhaifu, kivuli chake. Maadui zake waligundua siri hiyo kupitia kwa mke wake na kupanga njama.
Siku moja, adui zake walimshambulia wakati wa jua kali. Walilenga kivuli chake, na hapo ndipo nguvu zake zilipomwacha. Luanda Magere akaanguka na akafa.
jamii yake ilimkumbuka kama shujaa mkubwa, lakini kifo chake kilionyesha kuwa hata mashujaa wana udhaifu.
Sifa za Mighani
- Huwa ni hadithi za kishujaa
- Shujaa husalitiwa na mtu wake wa karibu
- Hueleza zaidi maughui ya uzalendo
- Huwa na migogoro kama vita auchangamoto
Umuhimu wa Mighani
- Huburudisha wasikilizaji
- Huelimisha kwa kutolea mafunzo
- Hukuza utambulisho wa jamii
Hekaya
Hekaya ni aina ya hadithi katika fasihi simulizi ambazo humhusu mhusika mmoja mwenye ujanja mwingi. Mhusika huyu hutumia akili na ujanja wake kujinufaisha au kuwashinda wengine.
Katika hekaya, mhusika mkuu mara nyingi huwa:
- Mjanja kuliko wengine
- Mwerevu na mwenye hila
- Hutumia akili badala ya nguvu
Abunuwasi na Karai
Siku moja,Abunuwasi alimwendea jirani yake akaomba amkopeshe karai ampe punda wake maji.Jirani alimpa bila kisita.Baada ya siku chache,Abunuwasi alirudisha karai hiyo akiwa ameongeza karai ndogo ndani yake.
Jirani alishangaa na kumuuliza kwa nini.Abumuwasi akamwambia,
”Karai yako imezaa.”
Jirani akafurahi sana na akapokea zote mbili.
Baadaye, Abunuwasi akaomba tena kukopa karai ile ile.Jirani, kwa matumaini ya faida nyingine akamkopesha.Safari hii,siku zilipita lakini Abunuwasi hakurudisha karai.
Jirani alipokwenda kuuliza, alimkuta Abunuwasi akiwa na huzuni kubwa. Abunuwasi akamwambia,
”Pole sana, karai yako ilifariki na nikaizika.”
Jirani alishangaa na kusema karai haiwezi kufa.Abunuwasi akamjibu,
”Kama karai inaweza kuzaa, basi inaweza pia kufa.”
Sifa za Hekaya
- Mhusika mmoja hutumia ujanja wake kujinufaisha
- Huwa na mhusika mmoja anayedhulumiwa
- Hutumia lugha nyepesi
Umuhimu wa Hekaya
- Hufundisha dhidi ya udanganyifu na tamaa
- Huburudisha wasikilizaji
- Hufundisha dhidi ya matumizi ya akili
Visasili
Visasili ni hadithi katika fasihi simulizi ambazo hueleza asili au chanzo cha jambo fulani katika jamii.Hadithi hizi hufafanua kwa nini kitu fulani kipo au kwa nini hali fulani hutokea.
Kwa mfano, visasili vinaweza kueleza:
- Chanzo cha mlima au mto
- Kwa nini wanyama fulani wana tabia maalum
- Asili ya desturi au imani fulani
Sungura na Kobe
Zamani sana, Sungura na Kobe walikuwa marafiki. Siku moja waligombania maji ya mto. Siku moja waligombania maji ya mto. Katika ugomvi huo, maji yakamwagika kila mahali na kuunda mito midogo mingi. Ndiyo maana hadi leo kuna mito mingi inayotiririka kutoka sehemu moja.
Sifa za Visasili
- Hueleza chanzo cha jambo
- Huwa na wahusika wa ajabu au wa kawaida k.v watu,wanyama au mizimu
- Huambatana na imani za jamii husika
Umuhimu wa Visasili
- Huburudisha na kufundisha
- Hutoe maelezo ya mambo yasiyoeleweka kwa urahisi
- Huhifadhi utamaduni na imani za jamii
Nyimbo
Nyimbo ni tungo za kisanaa zenye mahadhi ya kupanda na kushuka kwa sauti ambazo huimbwa.Huwa na mpangilio maalum wa maneno na sauti.
Aina za Nyimbo
Kuna aina nyingi za nyimbo.
- Bembelezi
- Nyimbo za Kazi
- Nyimbo za Dini
- Nyimbo za watoto
Bembelezi
Bembelezi ni nyimbo zinazoimbwa kwa watoto wadogo ili kuwabembeleza au kuwalaza.
Mfano
Sifa za Bembelezi
- Huimbwa kwa sauti ya upole
- Kuna urudiaji wa maneno au vifungu
- Huimbiwa watoto ili kuwaliwaza
- Huwa na maneno rahisi
Umuhimu wa Bembelezi
- Humtuliza mtoto
- Huonyesha upendo wa mzazi kwa mtoto
- Hukuza lugha kwa watoto
Nyimbo za Kazi
Hizi ni nyimbo zinazoimbwa wakati wa kufanya kazi kama kulima,kuvuna,kuvua na kujenga.
Sifa za Nyimbo za Kazi
- Huongeza ari ya kufanya kazi
- Huimbwa kwa pamoja
- Huwa na mdundo wa kuhamasisha
Umuhimu wa Nyimbo za Kazi
- Huleta mshikamano
- huondoa uchovu
- huongeza kasi ya kazi
Nyimbo za Dini
Hizi ni nyimbo zinazoimbwa katika shughuli za kidini kama ibada au sherehe za kiimani.
Mfano
Sifa za Nyimbo za Dini
- Huwa na maneno ya sifa au maombi
- Huonyesha imani ya jamii
- Huimbwa kwa heshima na utulivu
Umuhimu wa Nyimbo za Dini
- Huimarisha imani
- Hufundisha maadili
- Huleta utulivu wa moyo
Nyimbo za Watoto
Nyimbo za watoto ni nyimbo zinazoimbwa na watoto wakati wa kucheza,kujifunza au kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii.
Tofauti na bembelezi(zinazoimbwa na watu wazima kwa watoto), nyimbo za watoto huimbwa na watoto wenyewe.
Mfano
Sifa za Nyimbo za Watoto
- Huwa na maneno rahisi na ya kurudiarudia
- Huwa na mdundo wa kuchekesha au wa kucheza
- Mara nyingi huambatana na michezo au vitendo
- Huendeleza ubunifu na mshikamano.
Umuhimu wa Nyimbo za Watoto
- Huburudisha
- Hukuza lugha na msamiati kwa watoto
- Hufundisha maadili na nidhamu
- Huimarisha urafiki baina ya watoto