Teacher Resources

Teacher Resources

This section provides structured Kiswahili teaching resources for Junior School educators.It includes lesson plans, fasihi notes, assessment materials, and practical teaching strategies aligned with the CBC curriculum to support effective classroom instruction.

Walimu pia watapata uchambuzi wa kina wa kazi za fasihi andishi, ikiwemo novela, tamthilia na ushairi, ili kuwasaidia kuelewa na kufundisha maudhui, wahusika, dhamira na mtindo wa uandishi kwa urahisi zaidi. Matini haya yameandaliwa ili kuboresha uelewa wa wanafunzi na kuongeza ufanisi wa ufundishaji darasani.

Uchambuzi wa Novela

Uchambuzi wa Mji wa Matarajio

Katika sehemu hii tutashughulikia:

  • Utangulizi wa Novela ya Mji wa Matarajio.
  • Anwani Mji wa Matarajio.
  • Ploti na Mtiririko.
  • Maudhui au masuala makuu.
  • mbinu za uandishi
  • Sifa na umuhimu wa wahusika mbalimbali
  • Hitimisho ya Novela mji wa matarajio.

Utangulizi wa Novela ya Mji wa Matarajio

Mji wa Matarajio ni Novela inayoangazia maisha ya binti aliyeitwa Herina.Herina alikuwa Mwanafunzi aliyekuwa na matumaini ya kujiunga na gredi ya saba baada ya kufanya mtihani wa gredi ya sita.Lakini maisha yanachukua mkondo mwingine baada ya shangazi yake Dina kufika nyumbani kwao.

Baada ya matayarisho, walifunga safari moja kwa moja hadi Mji wa Matarajio ambako alikutana na mwajiri wake.Kazi yake ilikuwa ni kutunza mtoto mchanga.Anaifanya kazi hiyo kwa bidii na kwa kujitolea kwa moyo mmoja.Baadaye bidii yake inalipa na anaamua kurudi kuendelea na masomo yake.

Hiki ni kielelezo kizuri cha jinsi vijana wenye kiu ya elimu hupitia changamoto kabla ya kutimiza ndoto zao.

Anwani ya Mji wa Matarajio

Mji wa Matarajio ni ni madhari ambapo Herina alipelekwa na shangazi yake ili kupatana na mwajiri wake.Anwani hii pia ni anwani inayowakilisha Novela iliyojaa wahusika wnye matumaini mbalimbali.

  • Herina ana matarajio ya kujiunga na gredi ya saba katika shule ya upili ya Kileleni baada ya kufanya mtihani wa gredi ya sita
  • Herina alitarajia kurudi shuleni na kuendelea na masomo yake baada ya kumaliza kumtunza Jeff.
  • Herina alitarajia jeff apone.
  • Bi. na Bw. Makali walitarajia Herina aweze kurudi shuleni ili aendelea na kutimisha ndoto zake.
  • Bi. Makali alitarajia siku moja angepatana na Bwana Makali baada ya siku nyingi kwenda kazini.
  • Dina alikuwa na matarajio ya kuwa Bi Makali angepinga ombi lake la kuondoka na mwanawe Herina.
  • Jemima alitarajia kuwa angepata mfanyakazi mzuri ambaye angemtunza Jeff kwa upendo.
  • Jemima alikuwa na matarajio kuwa mwanawe angeweza kuapata uwezo wa kutembea na kuweza kuzungumza.

Ploti na Mtiririko wa Novela Mji wa Matarajio

Novela inaanza na binti mmoja anayeitwa Herina.Herina alikuwa tayari amekwisha kamilisha mtihani wa gredi ya sita na sasa alikuwa tayari kujiunga na gredi ya saba.Lakini sasa anakumbwa na matatizo mbalimbali.Mama yake Bi. Makali analalamika kuwa hawawezi kudhi mahitaji yake ya kujiunga na shule ya bweni ya kileleni.

Shangazi yake Dina anatokea na kumwarifu Bi. Makali ya kwamba alitaka mwanawe Herina aweze kuandamana naye hadi Mji wa Matarajio. Huko alikuwa amepata mwajiri ambaye aikuwa anahitaji msichana mbichi kama yeye.Msichana amabaye angeweza kuuza dukani kama vile Dina alivyodai.Baada ya muda wa matayarisho kabambe, Dina anarudi nyumbani kwa Bi. Makali kisha wanaondoka na Herina hadi mji wa Matarajio.

Wanapofika mji wa Matarajio, Herina anapatanishwa na mwajiri wake Jemima. Jemima alikuwa na mtoto mchanga, Jeff, ambaye aliitaji mlezi. Jeff alikuwa amekawia sana kabla ya kuzungumza na kuweza kutembea. Jemima alitarajia kuwa angempata kijakazi ambaye angeweza kumshughulikia Jeff bila kususia kazi kama vile awali walikuwa wamesusia.

Herina anachapa kazi kwa bidii na uvumilivu huku akitarajia kuwa siku moja angeweza kurudi nyumbani kujiunga na wazazi wake na baadaye kuweza kurudi shule na kuendelea na masomo yake.Jemima akiwa akiwa katika harakati za kufanya matibabu, anapatana na mgonjwa ambaye sasa, tunapata kumjua kama babake Herina ambaye alipata ajali katika shughuli zake za ujenzi.

Maudhui/Masuala makuu

Mwandishi wa Novela ya Mji wa Mtarajio amejikita katika maasuala mengi ambayo yanahusu jamii na mazingira yake.Yafuatayo ni baadhi ya maudhui ambayo yanapatikana katika Novela ya mji wa Matarajio.

  • Elimu
  • Dini
  • Umaskini
  • Mabadiliko
  • Teknolojia
  • Ajira ya Watoto
  • Majuto
  • Nafasi ya vijana katika jamii
  • Ajira

Mbinu za Uandishi

Methali

  • Haraka haraka haina baraka.
  • Hayawi hayawi huwa
  • Riziki ya Binadamu imo maishani mwake
  • Pilipili isioila yakuashiani?
  • Mzigo uko kichwani, kwapa lakutokeani jasho?…41
  • Ajali haina kinga
  • Wema hauozi
  • Mganga hajigangi…
  • lisilo budi hutendwa…uk 4
  • Kujikuna ujipatapo…uk 1
  • Juhudi za mfa maji uk 5
  • Ng,ombe maskini hazai pach uk…12
  • Dau la mnyonge haliendi joshi…uk 12
  • Jambo usilojua ni usiku wa giza…uk 8
  • Riziki ya binadamu imo maishani mwake…uk 11
  • Mtu hakatai mwito, hukataa aitiwalo…uk 20
  • Mjumbe mara zote hauwawi…uk 20
  • Kamba ya mbali haifungi kuni…uk 30
  • Ameshikwa na bila shaka, ilikuwa sharti ashikamane (ukishikwa shikamana)…uk 31
  • Riziki i mikononi mwa waja…uk 32
  • itabidi ajikune ajipatapo (mtu hujikuna ajipatapo)….uk 32
  • Kuku mgeni hakosi kamba mguuni…uk 33
  • Mwenye macho haambiwi tazama….uk 33
  • Pilipili usiyoila yakuashiani?…uk 41
  • Haraka haraka haina baraka…uk 47
  • Mhitaji ni mtumwa….uk 47
  • Mazungumzo yasiyomhusu ndewe wala sikio…uk 53
  • Msafiri na mara zote msafiri ni kafiri…uk 54
  • Chema chajiuza kibaya chajitembeza…uk 58
  • Hakika penye nia pana njia….uk 62

Nahau

  • Kupiga Deki
  • Kupanga vitu
  • Pigwa na butwaa…uk 5
  • Ridhia ombi…uk 1
  • Kuwa na macho ya kipanga…uk 6
  • Ishi pua na mdomo….uk 2
  • Kupinga rai kwa jino na ukucha…uk 2
  • Hakufa moyo….uk 3
  • Kata tamaa…uk 6
  • Kupigwa na butwaa…uk 8
  • Aliupiga moyo konde…uk 8
  • Alipiga dua…uk 8
  • Piga soga…uk 9
  • Hakuwaonea kijicho…uk 9
  • Shika tama…uk 12
  • Wameshika tariki…uk 15
  • Kufyata ulimi…uk 19
  • Kung’oa nanga…uk 19
  • Kutilia vizingiti…uk 19
  • Kutiwa mbaroni…uk 19
  • Tumevunjika moyo…uk 21
  • Ameghairi nia…uk 21
  • Kumtia soni…uk 24
  • Alitikisa kichwa…uk 40
  • Kushika tama…uk 41
  • Kjitafutia njuga…uk 42
  • Kutia kwenye ratili…uk 43
  • Kupiga foleni…uk 48
  • Kughairi nia…uk 50
  • Kuvaa tabasamu…uk 50
  • Kuvalia njuga…uk 50
  • Kimeng’oa nanga…uk 52
  • Kutia nanga…uk 55
  • Lililikupiga pambaja…uk 55
  • Ilifika ukingoni…uk 55
  • Kugonga mwamba…uk 61
  • Kutifua vumbi…uk 59
  • Jino na ukucha…uk 59
  • Kushusha pumzi ndefu…uk 67
  • Kupiga kidoko hafifu…uk 67
  • Alisafisha koo…uk 67
  • Kutikisa kichwa…uk 69
  • Kupinga chenga…uk 70
  • Kupiga deki…uk 72
  • Kumpungia mkono…uk 78
  • Amepiga hatua kubwa…uk 80
  • Akitikisa kichwa…uk 81
  • Kuutia mguu…uk 84
  • Kusimama dede…uk 84
  • Kupata afueni…uk 85
  • Kuambulia patupu…uk 86
  • Kushusha pumzi…uk 88
  • Tikisa kichwa…uk 89

Tashihisi

  • Roho ilimwenda mbio…uk 3
  • Maisha ya Herina yalitwaa sura mpya…uk 7
  • Ndege mmoja amwambie siri yake Dina…uk 8
  • Uso ulikuwa umejiandika…uk 9
  • Maini yalimkatika…uk 10
  • Moyo ulimsukuma
  • Akili yake ilimwambia…uk 11
  • Macho yalimuuliza…uk 21
  • Akili yake ilimwambia…uk 34
  • Moyo wake kumwenda mbio
  • Akili yake ilimtuma
  • Moyo wake uligjutuka ghafla…uk 50
  • Kutapika abiriria…uk 50
  • Garimoshi lilitafuna…uk 52
  • Moyo wake ulimkataza…uk 55
  • Joto ikitoroka…uk 59
  • Macho yake yamesalimu…uk 62
  • Macho kupiga chenga…uk 70
  • Mshangao uliojiandika usoni mwake…uk 70

Tashbihi

  • Siku zilijikokota mithili ya kobe
  • Akili inayoshika mambo kama sumaku
  • Rai yao kwa mwenyezi Mungu ilifanana kama shilingi kwa ya pili
  • Baada ya kuku kumeza punje ya mtama
  • Kichwa chake kilikuwa kimefura mithili ya ham**
  • Garimoshi lilitafuna masafa kama mja mwenye njaa
  • Shika mambo kama sumaku…uk 2
  • Siku zilijikokota mithili ya kobe…uk 11
  • Kujiona kama dalali aliyempiga bei mwanawe…uk 11
  • Kukutumia kama mtaji…uk 13
  • Alijihisi kama aliyeshindwa katika michezo ya miereka…uk 18
  • Moyo mzito kama nanga…uk 15
  • Wamebaidika kama mbingu na ardhi…uk 20
  • Kuwaongoza wawili hao kama mchungaji anayewaongoza kondoo malishoni…uk 28
  • Kushusha pumzi ndefu kama aliyeteua mzigo mzito…uk 42
  • Nyuso za waja hawa zilikuwa zimeganda kama barafu…uk 41
  • Aliwaona kama sisimizi…uk 48
  • Hata homa ya mkunguru ilikuwa imeadimika kwake kama wali wa daku…uk 49
  • Garimoshi lilitafuna masafa kama mja mwenye njaa…uk 52
  • Gari jilo lilifanana kama tui na maziwa…uk 57
  • Wawili walionekana kama makundi mawili ambayo yalikuwa yanacheza jungwe…uk 62
  • Shuka nyeupe kama theluji…uk 59
  • Kujiongeza hadhi kama kiumbe…uk 74
  • Nimekuletea mgeni, msichana mrembo na anayependeza kama wewe…uk 78
  • Kichwa chake kilikuwa kimefura mithili ya hamira…uk 85
  • Walisabahiana kama pacha…uk 92
  • Alilia kama mtoto mdogo…uk 81

Tutaendelea…

Ushairi

Maana ya Ushairi

Ushairi ni utungo wa kisanaa wenye mahadhi ya kupanda na kushuka kwa sauti ambo hughanwa.

Mambo Muhimu ya kuzingatia katika Ushairi

  • Dhamira
  • Maudhui
  • Wahusika
  • Nafsineni
  • Nafsinenewa
  • Muundo
  • Uhuru wa mshairi




Dhamira

Dhamira huwa ni lengo kuu la mwandishi. Dhamira huwa moja.

Maudhui

Maudhui huwa ni masuala makuu ambayo mwandishi anajikita nayo ili kuweza kueleza dhamira yake. Maudhui huwa ni mengi. Mfano, Maudhui ya Elimu,kazi,Familia,Teknolojia,utamaduni n.k.

Wahusika

Wahusika ni viumbe wanaotumiwa na mwandishi kuwasilisha maudhui na dhamira. Wahusika wanaweza kuwa wanadamu, wanyama, mizimwi, malaika au hata viumbe visivyo uhai.

Nafsineni

Nafsineni ni sauti ya anayezungumza katika shairi. Nafsineni anawezakuwa, mama, baba, mwalimu, mwanafunzi, daktari, mwanasiasa, mkulima, mpishi n.k.

Nafsinenewa

Nafsinenewa ni sauti ya anayezungumziwa katika shairi. Nafsinenewa anaweza kuwa, mama, baba, mwalimu, mtoto, mwanafunzi,daktari, mwanasiasa, mkulima, mpishi n.k.

Muundo

Muundo wa shairi umejikita katika vipengele mbalimbali.

  • Beti
  • Mishororo
  • Vipande
  • Vina
  • Mizani
  • Kibwagizo

Mfano wa Shairi

Beti

Shairi huwa limegawanywa katika beti.Umoja wa Beti ni ubeti.Shairi katika mfano wetu lina Beti nne.

Mishororo

Mishororo ni mistari ambayo hujenga Beti. Aina ya Shairi hujikita katika mishororo ambayo Iko katika Beti

mfano.

  • Shairi lenye mishororo miwili huitwa Tathnia
  • Shairi lenye mishororo mitatu huitwa Tathlitha
  • Shairi lenye mishororo minne huitwa Tarbia
  • Shairi lenye mishororo mitano huitwa Tahkmisa
  • Shairi lenye mishororo sita huitwa usita
  • Shairi lenye mishororo saba huitwa Usaba
  • Shairi lenye mishororo nane huitwa Unane

Vipande

Mishororo hugawanywa katika vipande.Kuna shairi ambazo huwa na;

  • Kipande kimoja huitwa utenzi
  • Shairi lenye vipande viwili huitwa mathnawi
  • Shairi lenye vipande vitatu huitwa ukawafi

Vipande mbalimbali huwa na majina.

  • Kipande cha kwanza huitwa ukwapi
  • Kipande cha pili huitwa utao
  • Kipande cha tatu huitwa mwandamizi

Vina

Vina ni silabi za mwisho katika kila kipande.Umoja wa vina ni Kina.

Ufuatao ni mpangilio wa vina katika shairi mbalimbali;

a)Mtiririko

Shairi la ina la mtiririko ni shairi ambalo vina vya kati na vya nje vinafanana kutoka ubeti mmoja hadi mwingine.

Mfano

Tukizingatia mfano huo tunaona kuwa vina vya kati vinafanana katika kila ubeti, vilevile vina vya nje ambavyo pia vinafanana.

b) Ukara

Kwenye ukara, vina vya kati/vina vya nje vinaweza kuwa vinatiririka kisha vya nje/vina vya kati vinabadilikabadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine.

Mfano

......ze,.....bu
.....ze,.....bu ubeti 1
.....ze,.....bu
..........

.....ze,.....a
.....ze,.....a ubeti 2
.....ze,.....a
..........

.....ze,.....ka
.....ze,.....ka ubeti 3
.....ze,.....ka
..........

.....ze,.....ta
.....ze,.....ta ubeti 4
.....ze,.....ta
..........

Kupitia mfano huo, vina vya kati (za) vinafanana katika kila ubeti ila vina vya nje vinabadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine.

c) Ukaraguni

Kwenye ukaraguni, vina vyote hubadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine.Kila ubeti una vina vyake tofautia na beti zingine.

mfano

.....ti,.....ko
.....ti,.....ko ubeti 1
.....ti,.....ko
..........

.....mba,.....pe
.....mba,.....pe ubeti 2
.....mba,.....pe
..........

.....me,.....si
.....me,.....si ubeti 3
.....me,.....si
..........

.....ku,.....ra
.....ku,.....ra ubeti 4
.....ku,.....ra
..........




Scroll to Top